Dar es salaam. Naibu waziri wa afya Dk.Faustine Ndugulile ameitaka Bodi mpya ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kumaliza tofauti zilizopo kati ya ofisi hiyo na taasisi nyingine.
Pia Dk. Ndugulile aliitaka ofisi ya mkemia mkuu kumaliza kazi kwa wakati kwa kuwa kuchelewesha kwa majibu ya vinasaba kutasababisha kuchelewa kupatikana kwa haki.
Alitoa maagizo hayo jana wakati akizindua bodi tendaji ya kwanza ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali.
"Nendeni mkakae chini na taasisi kama mamlaka ya chakua na dawa (TFDA), Shirika la viwango Tanzania (TBS) mkaangalie namna ya kumaliza tofauti zenu za kiutendaji" Alisema Dr. Ndugulile.
Naye mkemia mkuu wa serikali Dk.Fidelice Mafumiko alisema licha ya kuwepo kwa uwezo wa mamlaka kutimiza majukumu yake kumekuwepo na changamoto kadhaa zinazotakiwa kupewa ufumbuzi ili kujiimarisha kiutendaji.
Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Profesa esther Jason alisema atasimamia na kutekeleza yale yote waliyoelekezwa.
0 comments: