Thursday, 9 February 2017

MAKONDA NA MNYETI KUITWA BUNGENI..KURA ZOTE "NDIOO"

Kilichojili kipya bungeni Dodoma hapo jana February 8,2017 ni juu ya matumizi mabaya ya lugha kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mheshimiwa Paul makonda na mkuu wa wilaya ya
Arumeru mheshimiwa Alexander mnyeti kwa kile kiliichoitwa na wabunge kuwa ni ukosefu wa maadili kwa lugha walizozitumia waheshimiwa hao kukiongelea chombo hicho. Hali iliyopelekea wabunge kutaka waweze kuitwa katika kamati ya maadili ya bunge kwa madai ya kulidhalilisha bunge.
  
Makonda mbele ya waandishi wa habari

Awali waheshimiwa wabunge waliomba mwongozo kutoka kwa mwenyekiti wa bunge Andrew chenge kukubali bunge lijadili kuhusu kauli za mheshimiwa Paul makonda aliyetuhumiwa kwa kunukuliwa kauli yake wakati akiwazungumzia wabunge "Unajua zile ni mbwembwe tu, wakati mwingine wale huwa wanachoka na kusinzia hivyo inahitajika kuwe na watu wa kuwasaidia kucheka" alinukuliwa mkuu huyo.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru nae alirekodiwa sauti akisikika kukashifu utendaji kazi wa wabunge, bunge pia liliafiki ajumuishwe katika tuhuma hizo na kuitwa kwenye kamati ya bunge ya maadili. Mwenyekiti wa bunge Andrew chenge aliruhusu wabunge kupiga kura za "Ndio" au "Hapana" kuhusu makubaliano ya watuhumiwa wote kuitwa kwenye kamati ya maadili ya bunge ambapo kura zote zilikuwa za "Ndio"
 Baadhi ya wabunge wakiwemo Abdallah Ulega, Ester Bulaya, Mwita Waitara pamoja na Joseph Msukuma walisimama kuelezea Bunge namna walivyozipokea taarifa za Makonda huku wakiendelea kushinikiza bunge lizipokee hoja na kutaka kamati ya maadili itekeleze wajibu wake wa kumtaka kufika bungeni kwa ajili ya mahojiano.




0 comments: