Monday, 25 December 2017

HII NI SIRI NZITO YA MAFANIKIO YA ASKOFU GWAJIMA!!!!


"Chochote kile kinachoitwa kinyonge na kuonekana kinyonge kisidharauliwe kamwe". Ni maneno ya askofu gwajima aliyoyasema jana jumatatu tarehe 25.12.2017 katika ibada ya krismas kanisani kwake jijini Dar es Salaam.

Aliendelea kusema kuwa "hata yesu alizaliwa sehemu ya hori la kulishia ng'ombe lakini ndiye mkombozi wetu leo" 

Ogopa sana kilichozaliwa katika hori na ukiona mtu ameanzia juu jua tu ipo siku atashuka chini.

Askofu gwajima ansema kwamba ingewezekana yesu kuzaliwa sehemu ya heshima lakini MUNGU alipanga iwe hivyo ili kudhihirisha utukufu wake mkuu kwamba kilichozaliwa kwenye hori la ng'ombe ni chenye heshima na kikuu.

Kajitolea mfano wake halisi wa maisha yake kuwa hata yeye alianza kwa kuuza mihogo na barafu.

Askofu gwajima aliwatia moyo waumini wake ambao wapo katika hatua ya chini kabisa ya maisha wasije kukataa tamaa kwani kuna wakati MUNGU atawainua juu na wataheshimika.

"Niwaambie tu msiogope, alieanza kwa udhaifu atamaliza kwa heshima" aliyasema hayo askofu gwajima katika ibada ya krismasi kanisani kwake.

Amewataka pia kujenga tabia ya kuwasikiliza  hata wale aliowataja kuwa ni watu wa kuongeaongea tu kwani ipo sku MUNGU atawatumia kuwainua walio wanyonge.

0 comments: